• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi mjini Berlin ampiga risasi aliyekuwa anashambulia watu kwa kisu

    (GMT+08:00) 2018-06-04 08:55:18

    Polisi mjini Berlin wamempigia risasi mtu aliyekuwa anajaribu kuwashambulia watu kwa kisu katikati ya mji huo. Polisi wamesema tukio hilo lilitokea jana kwenye kanisa kuu la Berlin, na mshambuliaji alipigwa risasi mguuni, lakini wamesema tukio hilo halina uhusiano na ugaidi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ujerumani DPA, mshukiwa ni raia wa Austria mwenye umri wa miaka 53, alipelekwa hospitali baada ya kupigwa risasi na ofisa mmoja wa polisi pia alijeruhiwa kwenye tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako