• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgororo wa ushuru kati ya Mexico na Marekani watajwa kuwa huenda utavunja NAFTA

    (GMT+08:00) 2018-06-04 08:55:37

    Taasisi ya maendeleo ya viwanda na ukuaji wa uchumi IDIC imesema mgogoro wa ushuru unaozidi kupamba moto kati ya Mexico na Marekani, huenda unaweza kuvunja Makubaliano ya Biashara huria ya Amerika Kaskazini NAFTA. Kwenye ripoti yake mpya kuhusu kujenga upya ruwaza ya Mexico, taasisi hiyo imesema Mexico inapaswa kujiandaa kukabiliana na kuvunjika kwa Makubaliano ya biashara huria NAFTA, yaliyotekelezwa kwa miaka 25 kati ya Canada, Mexico na Marekani. Kabla ya hapo, rais Donald Trump wa Marekani ambaye anaamini kuwa makubaliano hayo yameharibu maslahi ya Marekani, alitaka makubaliano hayo yapitiwe upya ili kuinufaisha zaidi Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako