• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Libya mashariki mwa nchi launga mkono serikali ya mpito baada ya makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2018-06-04 08:55:56

    Serikali ya mpito ya Libya mashariki mwa nchi imetangaza kuwa bunge la Libya mashariki mwa nchi litaiunga mkono serikali hiyo kupitia "mipango mipya" ili kuondoa vizuizi vilivyoko kwenye makubaliano ya kisiasa yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa ambayo yalisainiwa mwaka 2015. Tangazo hilo limekuja siku kadhaa baada ya Mkutano uliokutanisha pande mbalimbali za kisiasa nchini Libya kufanyika mjini Paris, kujadili ufumbuzi wa msukosuko wa kisiasa nchini humo. Taarifa iliyotolewa na serikali hiyo inasema mipango mipya kuhusu kazi za serikali na benki kuu ya Libya itatangazwa katikati ya mwezi Juni baada ya kumalizika kwa mwezi mtakatifu wa Ramadhani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako