• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanyarwanda waandamana kuhimiza marufuku ya matumizi ya plastiki

    (GMT+08:00) 2018-06-04 09:09:06

    Mamia ya wanyarwanda jana waliandamana mjini Kigali kuhimiza umma kushiriki kwenye juhudi za kupambana na tatizo la uchafuzi wa plastiki. Maandamano hayo yaliyoandaliwa na wizara ya mazingira ya Rwanda kupitia mamlaka ya usimamizi wa mazingira REMA, ni sehemu ya shughuli za wiki ya mazingira na siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa kesho tarehe 5 Juni.

    Mkurugenzi mtendaji wa REMA Bibi Coletha Ruhamya amewahimiza wanyarwanda kukataa matumizi ya vitu vya plastiki vinavyotumiwa mara moja tu kama mirija, vikombe, sahani na chupa na kutafuta mbadala endelevu.

    Mwaka 2008 Rwanda ilipitisha sheria ya kupiga marufuku uagizaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, na kuweka faini kubwa kwa wale wanaotumia au kuiingiza kinyemela mifuko hiyo nchini Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako