• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yalishambulia kundi la Hamas kujibu mashambulizi ya maroketi

    (GMT+08:00) 2018-06-04 09:19:10

    Jeshi la anga la Israel jana usiku lilifanya mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza kwa mara ya tatu, wakati mgogoro kati ya Israel na wapiganaji wa gaza ukiendelea kuongezeka.

    Msemaji wa jeshi la Israel ametoa taarifa akithibitisha ndege za kivita za Israel kushambulia shabaha 15 huko Gaza, na kusema mashambulizi hayo ni kulipiza kisasi dhidi ya kitendo cha Hamas kuishambulia Israel kwa maroketi.

    Msemaji huyo amesema jeshi la Israel limeshambulia kituo cha kutengeneza na kuhifadhi maroketi na silaha katikati ya Gaza, na shabaha nyingine zilizoko kusini mwa Gaza.

    Tangu usiku wa jumamosi, mapambano kati ya Gaza na Israel yamerejeha baada ya kutulia kwa siku kadhaa, na kutishia kuvunja usimamishaji mapambano wa wiki iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako