• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaitaka jumuiya ya kimataifa kulaani Marekani kujitoa makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2018-06-04 09:45:58

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif ameihimiza jumuiya ya kimataifa kulaani kitendo cha Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA.

    Bw. Zarif amesema kitendo cha Marekani "cha upande mmoja na kisicho halali", kimetoa changamoto dhidi ya malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, na ufanisi wa mashirika ya kimataifa, na kinalenga kukiuka na kudhoofisha makubaliano hayo na azimio namba 2231 la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi wa Julai mwaka 2015.

    Bw. Zarif pia amesisitiza kuwa makubaliano ya JCPOA yaliyofikiwa baada ya mazungumzo yenye uwiano kati ya pande nyingine, yamekomesha msukosuko usio wa lazima uliodumu kwa zaidi ya miaka 10.

    Habari pia zinasema, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atafanya ziara barani Ulaya na kukutana na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, kujadili namna ya kuendelea kuzuia mpango wa nyuklia wa Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako