• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Wanawake-Rwanda: Timu ya AS Kigali yashinda ubingwa wa ligi kuu

  (GMT+08:00) 2018-06-04 09:49:32

  Timu ya soka ya wanawake ya AS Kigali imefanikiwa kutetea ubingwa wa ligi kuu nchini Rwanda baada ya kufikisha pointi 39 katika mechi 14 ilizocheza msimu, na ikiwa imeshinda mechi 13 na kushindwa mechi moja tu.

  Katika mechi yao ya mwisho msimu huu, AS Kigali iliwashinda Scandinavia kwa goli 1-0 ikiwa ugenini wilayani Rubavu, na sasa timu hiyo inatwaa ubingwa huo kwa mara ya 10 mfululizo.

  Kwa ubingwa huo, AS Kigali imekabidhiwa kombe na zawadi ya fedha taslimu, faranga za Rwanda milioni 1.

  Wachezaji Anne Nibagwire wa timu ya Scandinavia na Calixte Iradukunda wa AS Kigali wameibuka wafungaji bora msimu huu baada ya kila mmoja kufunga magoli 12.

  Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizopigwa mwishoni mwa juma hili, Rambura iliifunga Gakenke 2-0, Bugesera ikaifunga Kamonyi 3-0 na Inyemera ikishinda dhidi ya ES Mutunda kwa 3-0.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako