• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Matumizi ya Kadi ya Kijani: Nchi zisizo wanachama wa FIFA zaanza rasmi kuitumia

    (GMT+08:00) 2018-06-04 10:01:05

    Tofauti na ilivyozoeleka katika mchezo wa mpira wa miguu, ambapo adhabu zitolewazo na mwamuzi kutokana na makosa uwanjani huongozwa na kadi za aina mbili, ya manjano ambayo ni onyo, na nyekundu ambayo humuondoa mchezaji uwanjani, vyama visivyo wanachama wa FIFA vimeanza matumizi rasmi ya kadi ya rangi ya kijani.

    Kadi ya kijani ambayo inatumika hususani mchezaji anapofanya udanganyifu wa kujirusha ili kumhadaa mwamuzi, humuondoa mchezaji muda huo huo uwanjani lakini hutoa nafasi kwa timu husika kumwingiza mchezaji mwingine badala yake.

    Kadi hiyo kwa mara ya kwanza imetumika kwenye michuano ya kombe la dunia kwa vyama vya soka ambavyo si wanachama wa FIFA, CONIFA inayoendelea mjini London nchini Uingereza, na kadi ya kwanza ikitolewa na mwamuzi kwenye mechi kati ya Padania na Tuvalu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako