• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Mechi za Kimataifa za Kirafiki: Neymar aisaidia Brazil kupata ushindi dhidi ya Croatia

    (GMT+08:00) 2018-06-04 10:01:22

    Baada ya kuwa majeruhi kwa muda wa miezi mitatu, mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar Dos Santos, jana amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza na kufunga goli muhimu la kwanza kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Croatia iliyopigwa mjini London.

    Neyma aliingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 46 matokeo yakiwa ni sare ya bila kufungana, Neymar aliipatia Brazil goli la kuongoza katika dakika ya 69, kabla ya Roberto Firmino aliyeingia pia akitokea benchi kuongeza la pili katika dakika ya 90.

    Katika mechi nyingine za kirafiki zilizopigwa jana Ureno ilitoka sare ya bila kufungana na Ubeligiji, Iceland ikaifunga Marekani kwa magoli 2-1, Niger ikishinda 2-0 dhidi ya Uganda na Mexico ikipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Scotland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako