• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia, Bado siku 10: Jina la Morocco lapokelewa, kushiriki kura Juni 13 kwa ajili 2026

    (GMT+08:00) 2018-06-04 10:01:47

    Kamati ya ngazi ya juu ya FIFA iliyokuwa na jukumu la kwenda kufanya kukagua miundo mbinu na usalama kwenye nchi 4 zilizoomba kuwa wenyeji wa michuano kombe la dunia mwaka 2026, imepitisha ombi la Morocco licha ya Changamoto zilizobainishwa na kuleta walakini kuhusu utayari wa nchi hiyo.

    Morocco sasa inasubiri zoezi la wajumbe wa mkutano mkuu kupiga kura ili kumpata mwenyeji wa michuano hiyo ambayo mara hiyo itahusisha timu 48.

    Kamati hiyo imedai Morocco ina upungufu katika maeneo muhimu matatu;

    1. Morocco imesema itaandaa viwanja 14 kwa ajili ya michuano hiyo, ambapo kati ya hivyo mpaka sasa haijaanza kujenga viwanja vipya 9, na hata hivyo vingine 5 vilivyopo havijaanza kufanyiwa ukarabati muhimu ili kufikia viwango

    2. Maeneo ya malazi bora yaliyopo karibu na viwanja ni machache kulingana na kanuni za FIFA zinavyoelekeza.

    3. Miundo mbinu ya Usafiri kutoka maeneo ya malazi ya timu na mashabiki kwenda viwanjani bado ni changamoto.

    Hata hivyo kamati hiyo iliyo chini ya katibu mkuu wa FIFA, Bi Fatma Samoura, imepitisha jina la Morocco, baada ya kufanya mkutano na kamati ya kitaifa ya maandalizi, pamoja na Serikali Kuu ya Morocco ambayo imeahidi kuwa imetenga fedha kwa ajili ya maandalizi, na kazi hiyo itakamilika kabla ya mwaka 2026.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako