• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara itakayofanywa na rais wa Russia nchini China yatajwa kuwa na umuhimu mkubwa

    (GMT+08:00) 2018-06-04 10:15:56

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema ziara itakayofanywa na rais Vladimir Putin wa Russia nchini China ni muhimu katika kupanga hatua zijazo za kukuza uhusiano kati ya China na Russia.

    Bw. Wang Yi amesema hayo mjini Johanesburg wakati alipokutana na mwenzake wa Russia Bw. Sergei Lavrov, kando ya mkutano rasmi wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la BRICS.

    Rais Putin anatarajiwa kufanya ziara nchini China kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 10 mwezi Juni na kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai SCO utakaofanyika huko Qingdao. Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya Rais Putin katika awamu yake mpya ya urais, na itakuwa ni mara ya kwanza kwa marais hao kukutana kwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako