• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini na Marekani wajadili mkutano wa kilele kati ya Korea Kaskazini na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-06-04 10:41:39

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini na Marekani wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu kujadili mkutano wa kilele unaotarajiwa kufanyika kati ya kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un na rais Donald Trump wa Marekani.

    Kwenye mazungumzo yao, waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Bw. Kang Kyung-wha na mwenzake wa Marekani Bw. Mike Pompeo wamebadilishana maoni kuhusu maendeleo mapya ya maandalizi ya mkutano huo wa kilele, ikiwemo ziara ya naibu mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Chama Tawala cha Wafanyakazi cha Korea Kaskazini Bw. Kim Yong Chol nchini Marekani, na kukutana na rais Donald Trump.

    Baada ya kukutana na ofisa huyo mwandamizi wa Korea Kaskazini, Ijumaa iliyopita rais Trump alisema atakutana na Bw. Kim Jong Un tarehe 12, Juni nchini Singapore kama ilivyopangwa.

    Bw. Kang na Bw. Pompeo wamefanya majadiliano ya kina kuhusu jinsi ya kuufanikisha mkutano huo wa kilele kati ya Korea Kaskazini na Marekani, na kukubaliana kufanya mashauriano ya karibu na kutafuta njia za kutimiza malengo ya kuondoa silaha za kinyuklia kwenye Peninsuala ya Korea na kuleta amani ya kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako