• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa China na Uingereza waona China inapiga hatua kubwa katika kuwa nchi yenye nguvu ya kulinda hakimiliki ya ujuzi

    (GMT+08:00) 2018-06-04 16:58:31

    Mwaka 2008 China iliweka Mwongozo wa mikakati kuhusu hakimiliki ya ujuzi, ambao ni waraka unaotoa maelekezo ya kuijenga China kuwa nchi ya uvumbuzi. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alifanya mahojiano na wataalamu wa China na Uingereza, ambao wanaona katika miaka kumi iliyopita China imefanya juhudi kubwa katika kulinda hakimiliki ya ujuzi, na maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta hiyo, yameweka msingi muhimu katika kuihimiza China ikue na kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani.

    Katika miaka kumi iliyopita, China iliweka waraka wa kimwongozo unaohusu maendeleo ya mambo ya hakimiliki ya ujuzi. Baada ya juhudi za miaka kumi, China imepata mafanikio makubwa katika sekta hiyo na kufanya uvumbuzi kwa kujitegemea, hali ambayo imeweka mazingira tulivu, haki na wazi kwa mambo ya biashara. Mkurugenzi wa Kituo cha manunuzi ya serikali katika Chuo Kikuu cha Nottingham cha Uingereza Prof. Wang Ping, amesema hivi sasa utaratibu wa sheria kuhusu hakimiliki ya ujuzi umeboreshwa, hali ambayo imeweka msingi muhimu wa kisera kwa China kujiendeleza kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani. Anasema:

    "China imepata maendeleo makubwa katika kulinda hakimiliki ya ujuzi: sheria zinazohusika zimeboreshwa, na mahakama maalumu kuhusu hakimiliki imeanzishwa. Hadi sasa Uingereza bado haijawa na mahakama maalumu ya hakimiliki ya ujuzi."

    Mwenyekiti wa Klabu ya kundi la kampuni 48 ya Uingereza Bw. Stephen Perry ameeleza kuwa, endapo China itajiendeleza kuwa na kiwango cha katikati cha nchi iliyoendelea, inapaswa kuziongoza nchi nyingine katika sekta ya teknolojia na uvumbuzi. Bw. Perry anasema:

    "Hivi karibuni rais Xi Jinping wa China alisisitiza kuwa alama ya China ya kufikia kiwango cha katikati cha nchi zilizoendelea, ni kupata maendeleo makubwa katika kufanya uvumbuzi wa teknolojia. Ili kutimiza lengo hilo, China inapaswa kushikilia kithabiti sera ya kimsingi ya kufanya uvumbuzi. 'Made in China 2025' ni mkakati muhimu wa maendeleo kwa China, ni hadi lengo hilo litakapotimizwa, ndipo maendeleo ya kampuni za China yatakuwa na umuhimu zaidi, na zitaweza kufanya mazungumzo na ushirikiano kwa usawa na kampuni za nchi za magharibi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako