• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

    (GMT+08:00) 2018-06-04 17:14:58

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana huko Pretoria amekutana na mjumbe wa kitaifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje, Bw. Wang Yi.

    Rais Ramaphosa amesema, Afrika Kusini inatarajia rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za BRICS utakaofanyika mwezi Julai nchini Afrika Kusini na kufanya ziara nchini humo. Amesema anatumaini kuwa ziara hiyo itatoa fursa mpya kwa nchi hizo mbili kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati yao. Vilevile amesema Afrika Kusini inafurahi sana kupata fursa ya kushiriki kwenye maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zilizoagizwa nchini China yatakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu huko Shanghai.

    Kwa upande wake, Bw. Wang Yi amesema China na Afrika Kusini zinapaswa kuimarisha uratibu, uaminifu wa kisiasa, na ushirikiano wa kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako