• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya amani yasainiwa kati ya miji ya Misurata na Tawergha nchini Libya

    (GMT+08:00) 2018-06-04 17:25:43

    Miji ya Misurata na Tawergha nchini Libya imesaini makubaliano ya amani ambayo yanawaruhusu wakazi takriban elfu 40 wa Tawergha kurejea makwao baada ya kukimbia kwa miaka saba kutokana na kuunga mkono serikali ya zamani katika vurugu iliyotokea mwaka 2011.

    Mkuu wa baraza la serikali ya Misurata Bw. Mustafa Karwad amesema, makubaliano hayo yanalenga kufunga ukurasa wa zamani na wakazi wa jirani wa Tawergha na kuzuia pande nyingine kutumia suala hilo kupata faida za kisiasa au kikanda.

    Bw. Karwad ameongeza kuwa, ikiwa ni mwanzo na hatua nzuri inayowawezesha watu wote waliokimbia makazi yao kurejea, mapatano hayo ya amani yanatimizwa baada ya pande mbili kufikia makubaliano kwa lengo la kuanzisha kanuni za uhusiano mzuri wa ujirani kati ya walibya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako