• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa ulinzi wa Marekani asema nchi hiyo haitaondoa jeshi lake kutoka Peninsuala ya Korea ndani ya muda mfupi

    (GMT+08:00) 2018-06-04 18:27:10

    Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis amesema, nchi hiyo haitaondoa jeshi lake kutoka Peninsuala ya Korea katika siku za karibuni.

    Bw. Mattis amesema, suala la kuondoa jeshi la Marekani halipo kwenye mambo yanayojadiliwa kwa sasa, na kwamba baada ya miaka mitano au kumi huenda Marekani na Korea Kusini zitajadili tena suala hilo.

    Msaidizi maalumu wa mambo ya nje na ulinzi wa usalama wa rais wa Korea Kusini Bw. Moon Chung-in amesema, suala la Marekani kuondoa jeshi lake katika peninsula ya Korea linatakiwa kuangaliwa wakati makubaliano ya amani yatakaposainiwa. Msemaji wa ikulu ya Korea Kusini Bw. Kim Eui-kyeom amesema, rais Moon Jae-in ameweka bayana kuwa jeshi la Marekani nchini Korea Kusini ni suala la muungano wa Korea Kusini na Marekani, ambalo halihusiani na makubaliano ya amani.

    Habari nyingine zinasema, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inazitaka Korea Kaskazini na Korea Kusini kuendelea kuimarisha mazungumzo na kuboresha uhusiano. Pia amesema China inaunga mkono Korea Kaskazini na Marekani kuendelea kufanya juhudi ya pamoja, na kuhimiza kukamilisha maandalizi ya mkutano kati ya viongzi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako