• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zimbabwe yakataa madai ya Marekani kuhusu uchaguzi mkuu ujao nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-06-04 19:06:44

    Serikali ya Zimbabwe imesema imechukua hatua za kufaa za kiutendaji ili kuhakikisha uchaguzi wa Julai 30 unafanyika kwa uhuru, haki, na kuaminika.

    Kauli hiyo ni majibu kwa mbunge wa Marekani Chris Coons aliyesema kuwa utawala wa rais Emmerson Mnangagwa unatoa ahadi hewa na kuchelewesha kwa makusudi utekelezaji wa mageuzi muhimu ya mfumo wa uchaguzi ili kunyamazisha upinzani.

    Gazeti la The Herarld la Zimbabwe limemnukuu msemaji wa rais Mnangagwa, George Charamba akisema, serikali imehakikisha uchaguzi wa amani, ambao ni sababu ya rais kuwa muwazi kuhusu wito wake wa amani na pia katika kuchukua hatua ya kukutana na vyama vya upinzani mara baada ya Mahakama ya Uteuzi kuthibitisha nani ni halali na nani hafai kugombea.

    Wakati huohuo, vyama vya upinzani nchini Zimbabwe chini ya muungano wa MDC vinapanga kufanya maandamano hapo kesho kuilazimisha Tume ya Uchaguzi nchini humo (ZEC) kutekeleza mageuzi ya sheria ya uchaguzi kabla ya Julai 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako