• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qatar yaunga mkono serikali ya Sudan kurudisha mazungumzo ya amani ya Darfur

    (GMT+08:00) 2018-06-04 19:25:40

    Rais wa Sudan Bw. Omar al-Bashir amekutana na mjumbe maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Qatar Bw. Mutlaq Al Qahtani katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

    Bw. Qahtani amesema, Qatar inaunga mkono serikali ya Sudan kurudisha mazungumzo ya amani na vikundi vya wapiganaji vya Darfur kwa mujibu wa mkataba wa amani wa Doha kuhusu Darfur, ili kuisaidia Sudan kutimiza amani na kumaliza mchakato wa amani.

    Kamishna wa serikali ya Sudan anayeshughulikia eneo la Darfur Bw. Amin Hassan Omar, amesema serikali ya Sudan iko tayari kuanzisha mazungumzo ya amani ya Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako