• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Soko la maua la Marekani lina thamani ya Sh10bn

  (GMT+08:00) 2018-06-04 20:30:23

  Mapato ya Kenya kutoka soko la maua la Marekani, imesemekana kuongezeka hadi Sh bilioni 10 kwa ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi kuelekea New York iliyopangwa kuanza mwezi Oktoba.

  Mkurungezi mkuu wa baraza la Maua Kenya, Clement Tulezi amesema katika mahojiano kwamba nchi hivi sasa inapata chini ya bilioni kutoka soko la Marekani.

  Mapato kutoka sekta ya Maua ilifika Sh bilioni 115 mwaka jana kutoka Sh bilioni 101 mwaka 2016.

  Makampuni yaliyoidhinishwa kufanya mauzo ya nje pia yaliongezeka hadi 386 kutoka 356 mwaka 2016.

  Wakati Kenya imebaki muuzaji mkubwa wa mauzo ya nje ya maua Tulezi alibainisha kuwa wanakabiliwa na ushindani kutoka masoko kama vile Rwanda, Uganda, Zimbabwe, na Ethiopia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako