• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yataka maofisa wa ununuzi na wahasibu waachie ofisi zao ili uchunguzi ufanyike

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:10:26

    Kenya imewataka maofisa wa idara za manunuzi na wahasibu kwenye wizara mbalimbali, idara na mashirika ya serikali, waachie ofisi na kuwaachia nafasi manaibu wao, ili wafanyiwe ukaguzi.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Kenya Bw. Mwenda Njoka amesema maofisa waandamizi wa serikali watatakiwa kuchunguzwa mitindo yao ya maisha na kuwasilisha taarifa zao binafsi.

    Maagizo hayo yamekuja baada ya mwito uliotolewa wiki iliyopita na rais Uhuru Kenyatta, kuwafanyia ukaguzi mpya maofisa wa serikali ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ufisadi, baada ya kugunduliwa kwa kashfa ya upotevu wa dola milioni 90 za kimarekani za idara ya taifa ya huduma kwa vijana.

    Idara za manununzi za serikali ya Kenya na mashirika ya serikali yanatajwa kukithiri kwa tatizo la ufisadi nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako