• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WAHO yatoa mwito wa kuchukua tahadhari zaidi kuhusu Ebola

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:10:45

    Shirika la afya la nchi za Afrika Magharibi WAHO limetoa mwito kwa nchi za Afrika Magharibi kuwa kwenye tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola baada ya ugonjwa huo kutokea tena nchini DRC.

    Akiongea kwenye mkutano mjini Banjul, mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Bw. Stanley Okolo amesema kutokea kwa ugonjwa huo kunakumbusha nchi hizo kuendelea kuwa na tahadhari na kujiandaa. Bw. Okolo amesema tayari WAHO imetuma taarifa kwa nchi mbalimbali kuwakumbusha takwimu kuhusu ugonjwa huo na kanuni wanazotakiwa kufuata.

    Maofisa wa afya wa WAHO wanaendelea na mkutano kujadili matatizo ya afya ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa magonjwa na upungufu wa bajeti za afya, kabla ya mkutano wa 19 wa mawaziri wa nchi za ECOWAS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako