• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ikulu ya Marekani yasema Marais Trump na Kim watakutana saa 3 asubuhi ya Juni 12

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:11:09

    Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa mkutano kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, umepangwa kufanyika saa tatu asubuhi ya Juni 12 nchini Singapore.

    Msemaji wa ikulu ya Marekani Bibi Sarah Sanders amesema timu ya utangulizi ya Marekani tayari imewasili nchini Singapore kukamilisha mambo ya ugavi na itaendelea kuwepo huko hadi mkutano utakapoanza.

    Habari pia zinasema Shirika la kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA limesema liko tayari kukagua mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini, kama likiruhusiwa kutoa mchango muhimu baada ya makubaliano ya kisiasa kufikiwa.

    Mkurugenzi wa IAEA Bw. Yukiya Amano amesema timu ya IAEA iko tayari kufanya uchunguzi wa nyuklia nchini Korea Kaskazini, lakini uchunguzi huo unatakiwa kuwa chini ya makubaliano ya pande zinazohusika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako