• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan Kusini kufanya mazungumzo ya amani na kiongozi wa kundi la waasi

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:38:09

    Msemaji wa rais wa Sudan Kusini Bw Ateny Wek Ateny amesema rais Salva Kiir yuko tayari kufanya mazungumzo ya amani na kiongozi wa kundi la waasi Riek Machar.

    Bw. Ateny amesema rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amelikubali pendekezo la Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki IGAD, kufanya mazungumzo na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar kwa ajili ya kutimiza amani.

    Wiki iliyopita IGAD ilimpendekezea rais Kiir wa Sudan Kusini afanye mazungumzo na Bw. Machar kabla ya mkutano ujao wa kilele wa Umoja wa Afrika kufanyika mwezi Julai nchini Mauritania, ambayo mazungumzo hayo yatakuwa ya kwanza ya uso kwa uso kati yao tangu Bw. Machar alipokimbilia Juba mwezi Julai mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako