• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Msumbiji zasaini makubaliano yenye thamani ya dola za Marekani milioni 100

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:42:19

    Serikali za China na Msumbiji zimesaini makubaliano ya miradi minne yenye thamani ya dola za Marekani milioni 100 katika mkutano wa sita wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano wa kiuchumi, kiufundi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika mjini Maputo, Msumbiji.

    Pande hizo mbili zimepitia mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu mkutano wa tano wa tume hiyo ufanyike mwaka 2015, na kujadiliana kwa kina kuhusu kuimarisha ushirikiano katika mambo ya biashara, uwekezaji na msaada wa maendeleo..

    Habari zinasema, miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa chuo cha ufundi katiaka jimbo la Sofala, uwanja wa ndege wa Xai-Xai, ushirikiano wa kiufundi wa uwanja wa taifa na ushirikiano na mawasiliano ya wataalam wa kilimo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Msumbuji Bw. Jose Pacheco amesema tangu rais Philipe Nyusi afanye ziara nchini China mwaka 2016, uhusiano kati ya China na Msumbiji umeinuka na kufikia ngazi ya kimkakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako