• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 27 wa al-Shabaab wauawa kwenye shambulizi la anga Somalia

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:42:39

    Jeshi la Marekani limesema, kikosi maalum chake kimefanya shambulizi la anga kaskazini mwa Somalia na kuwaua magaidi 27 wa kundi la al- Shabab.

    Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika Africom imetoa taarifa kuwa, shambulizi hilo lilifanywa kwa kushirikiana na serikali ya Somalia katika eneo la magharibi la Bosasso. Taarifa hiyo imesema mpaka sasa hakuna ripoti kuhusu kuuawa kwa raia kwenye shambulizi hilo.

    Shambulizi hilo ni moja ya mashambulizi yanayofanywa na majeshi ya Marekani nchini Somalia kwa kushirikiana na jeshi la serikali na vikosi vya AMISOM, dhidi ya wapiganaji wa Al-Shabaab ambao bado wana ngome katika eneo la kusini mwa Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako