• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Michuano ya SportPesa: Simba yafuzu nusu fainali, yaiondoa Kariobangi

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:52:23

    MABINGWA wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, Simba wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 3-2 waliopata jana dhidi ya Kariobangi Sharks kufuatia matokeo ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

    Shujaa wa Simba alikuwa ni golikipa wake Aishi Salum Manula aliyeokoa penalti mbili za Kariobangi Sharks na sasa timu hiyo itakutana na Kakamega Homeboys katika Nusu Fainali.

    Waliofunga penalti za Simba SC ni Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni na Jonas Mkude, wakati Mohammed Hussein na Paul Bukaba walikosa.

    Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi kati ya Singida United ya Tanzania itamenyana na AFC Leopards ya Kenya na mshindi atakutana na Gor Mahia katika nusu fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako