• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tennis, Michuano ya Ufaransa: Serena ajiondoa kwenye mechi dhidi ya Sharapova

    (GMT+08:00) 2018-06-05 09:53:40

    Katika hali iliyoshtua mashabiki wa mchezo wa tennis kote duniani, mchezaji nyota kutoka Marekani Serena Williams alijitoa kwenye mchezo wa raundi ya nne kwenye michuano mikubwa ya Ufaransa mwaka huu inayoendelea mjini Paris.

    Katika mechi hiyo, Serena alitarajiwa kucheza na mpinzani wake wa siku nyingi Maria Sharapova ambaye sasa anafuzu robo fainali bila kupingwa.

    Serena aliwaambia waandishi wa habari kuwa, amejiondoa kwenye mechi hiyo kwa sababu ya maumivu ya misuli ya bega.

    Kwenye raundi inayofuata Maria atakutana na Garbine Muguruza wa Hispania ambaye naye alifuzu baada ya mpinzani wake Lesia Tsurenko aliyejiondoa kwa sababu ya majeruhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako