• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Putin asaini muswada kuwa sheria kukabiliana na vikwazo vya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-06-05 10:11:18

    Serikali ya Russia imesema rais Vladimir Putin amesaini muswada ambao sasa utakuwa sheria kamili, inayomruhusu kuchukua hatua kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani na "nchi nyingine zisizo za rafiki".

    Sheria hiyo inampa rais wa Russia madaraka ya kuzuia au kudhibiti ushirikiano na mashirika ya nchi zisizo rafiki, na mashirika ya kigeni yanaweza kuzuiwa kutoa huduma kwa serikali kuu na serikali za mitaa za Russia, kufanya biashara na mashirika ya Russia au kushiriki kwenye shughuli za ubinafsishaji wa mali za Russia.

    Hatua hiyo imekuja ili kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani mwezi Aprili dhidi ya watu binafsi na mashirika 38 ya Russia, wakiwemo viongozi saba wa biashara na maofisa waandamizi 17, kwa tuhuma za kuhusika na "shughuli za hujuma" kote duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako