• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Afrika Kusini wakutana Pretoria

    (GMT+08:00) 2018-06-05 10:52:30

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Afrika Bibi Lindiwe Silulu huko Pretoria. Kwenye mazungumzo yao Bw. Wang Yi amesema pande mbili zinatakiwa kuungana na kushirikiana kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS utakaofanyika nchini Afrika Kusini mwezi ujao, na mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika nchini China mwezi Septemba, ili kuhakikisha mikutano hiyo miwili inapata mafanikio, kuhimiza uhusiano wa kirafiki na kimkakati kati ya China na Afrika Kusini, kwenye msingi wa miaka 20 ya uhusiano wa kibalozi kati yao.

    Bw. Wang Yi ambaye anahudhuria mkutano wa mawaziri wa nchi za BRICS, amesema anaamini mkutano wa kilele wa FOCAC utainua kiwango cha uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema baraza hilo likiwa ni jukwaa muhimu la mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika, limekuwa mfano wa ushirikiano wa Kusini na Kusini na alama ya ushirikiano wa kimataifa na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako