• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazo la rais Xi Jinping wa China kuhusu maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira

    (GMT+08:00) 2018-06-05 13:03:24

    Ipo dunia moja tu ulimwenguni. Ni matumaini ya pamoja ya binadamu wote na jumuiya ya kimataifa kuhifadhi mazingira na kuhimiza masikilizano kati ya binadamu na mazingira. Matakwa ya watu yanaelekeza uongozi wa taifa.

    Katika miaka ya hivi karibuni, kwa mujibu wa wazo la kuhimiza maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira lililotolewa na rais Xi Jinping wa China miradi mbalimbali muhimu ikiwemo usimamizi wa mazingira na ufufuaji wa mazingira ya kiikolojia Ecological restoration imekuwa ikitekelezwa kwa utaratibu, mchakato wa kuundwa kwa mfumo wa mazingira yenye masikilizano umeharakishwa.

    Kutokana na mtizamo wa historia ya maendeleo ya dunia, kulinda mazingira ya ikolojia kunalinda uwezo wa uzalishaji, na kuboresha mazingira ya ikolojia kunaendeleza uwezo wa uzalishaji.

    ---Hotuba aliyoitoa rais Xi akifanya ukaguzi mkoani Hainan Aprili 10, mwaka 2013.

    "Mali ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu, lakini mito safi na milima yenye misitu vilevile ni muhimu sana kwa maisha yenye neema kubwa kwa watu, ambayo nafasi yake haiwezi kuchukuliwa na fedha. Je, utakuwa na furaha gani ukichuma pesa nyingi huku ukikosa hewa safi na maji salama ya kunywa? "

    Tunapaswa kugundua kuwa, milima, maji, misitu, mashamba na maziwa ni umoja wa maisha ambao unahusiana na kutegemeana kwa karibu, endapo moja kati yao inajishughulikia yenyewe na kupuuza nyingine, italeta uharibifu wa mfumo wa ikolojia. Kuna ulazima wa kubeba majukumu yote ya usimamizi, uhifadhi na ufufuaji wa maeneo yote ya ardhi ya taifa.

    ---Maelezo kuhusu Uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China juu ya masuala muhimu ya kuendeleza kwa pande zote mageuzi aliyoyatoa rais Xi Jinping kwenye Mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa awamu ya 18 wa chama cha kikomunisti cha China.

    Milima, maji, misitu, mashamba na maziwa ni umoja wa maisha. Rais Xi aliwahi kutoa ufafanuzi mzuri kwa umoja huo: "Milima ikiharibiwa na misitu ikikatwa, maji yakaharibiwa, milima ikawa tupu, na maji yakawa mafuriko, ardhi ikapoteza virutubisho, udongo utaporomoka."

    Uhifadhi wa mazingira ya ikolojia utanufaisha kizazi baada ya kizazi. Ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia unahusu neema ya wananchi na mustakabali wa taifa.

    ---Hii ni hotuba aliyoitoa rais Xi alipoendesha mafunzo ya sita katika Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha CPC.

    Kutokana na maelekezo ya wazo la rais Xi Jinping kuhusu kuendeleza maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira, China ikisimama katika mwanzo mpya wa historia, itaendelea kufuata wazo la ustaarabu wa ikolojia la kuheshimu, kufuatae, na kulinda mazingira kwa lengo la kuhusisha ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia katika sekta na mchakato wote wa ujenzi wa uchumi, siasa, utamaduni na jamii, ili kukabiliana na changamoto za ikolojia zinazoikabili dunia kwa kupitia utaratibu wa ushirikiano wa pande nyingi ikiwemo Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuijenga China kuwa na sura inayong'ara zaidi, na kutimiza maendeleo endelevu ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako