• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapata maendeleo makubwa katika kulinda hakimiliki ya ujuzi

    (GMT+08:00) 2018-06-05 16:55:39

    Kongamano la kuadhimisha miaka 10 tangu kutangazwa kwa "Mwongozo wa mikakati kuhusu hakimiliki ya ujuzi wa China" umefanyika leo hapa Beijing. Mwongozo huo uliotangazwa miaka 10 iliyopita na Baraza la serikali la China limeihusisha kazi ya kulinda hakimiliki ya ujuzi kwenye mikakati ya taifa, na maendeleo makubwa yamepatikana katika sekta hiyo.

    Katika miaka 10 iliyopita tangu "Mwongozo wa mikakati kuhusu hakimiliki ya ujuzi wa taifa" ulipotangazwa nchini China, kiwango cha China cha kulinda hakimiliki kimekuwa kikiinuka siku hadi siku, na China imekuwa nchi yenye uwezo mkubwa katika sekta hiyo. Takwimu zimeonesha kuwa, katika miaka 10 iliyopita, idadi ya vitu vilivyovumbuliwa na kupewa hakimiliki ya ujuzi imeongezeka kutoka elfu 96 mwaka 2007 hadi kufikia milioni 1.36 mwaka 2017, kiasi ambacho kinashika nafasi ya tatu duniani kikifuatia Marekani na Japan. Mkurugenzi wa Idara ya hakimiliki ya China Bw. Shen Changyu anasema:

    "Hadi sasa China imekuwa nchi ya kwanza duniani kutokana na idadi ya utoaji wa ombi la kupewa hakimiliki ya ujuzi ya China inayozidi milioni 1, pia imekuwa nchi ya tatu ikifuatia Marekani na Japan kutokana na idadi ya vitu vya kuvumbuliwa na kupewa hakimiliki inayozidi milioni 1, hali ambayo imethibitisha kuwa China imekuwa nchi kubwa ya hakimiliki ya ujuzi."

    Wakati huo huo, China imekuwa ikiongeza nguvu katika kulinda hakimiliki ya ujuzi. Tokea mwaka 2008, bunge la umma la China limerekebisha sheria mbalimbali zikiwemo hakimiliki, alama za bidhaa, na kupinga ushindani usio halali, na baraza la serikali pia limetunga na kurekebisha sheria mbalimbali zinazohusika. Mbali na hayo, China imekuwa ikipambana na vitendo vya kukiuka sheria ya hakimiliki ya ujuzi, kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2016, China imekamata bidhaa milioni 500 zinazokiuka sheria zinazohusu hakimiliki ya ujuzi.

    Mjumbe maalumu wa Kamati ya hukumu ya Mahakama kuu ya Umma Bw. Hu Yunteng ameeleza, katika miaka 10 iliyopita, China imeimarisha pande zote ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi, na pia imeanzisha mfumo wa sheria kuhusu hakimiliki ya ujuzi unaolingana na kanuni za kimataifa. Anasema:

    "Kuanzia mwaka 2009 hadi 2017, kesi laki 7.45 zinazohusu hakimiliki ya ujuzi zimekamilishwa kwenye mahakama hiyo, na wastani wa ongezeko umefikia asilimia 17.8 kwa mwaka, huku kiwango cha kesi zilizokamilishwa kikizidi asilimia 95."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako