• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyama vya CPC na ANC vyakubaliana kuongeza ushirikiano

    (GMT+08:00) 2018-06-05 18:20:30

    Ofisa wa ngazi ya juu wa Chama cha Kikomuniti cha China (CPC) Chen Xi ameahidi kuimarisha mawasiliano ya uzoefu wa uongozi na chama cha ANC cha Afrika Kusini ili kuboresha uhusiano wa pande mbili.

    Chen ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la CPC na mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya Kamati Kuu ya CPC ametoa kauli hiyo alipokutana na ujumbe wa Chama cha ANC unaoongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Elias Magashule.

    Chen amesema, huu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa pande mbili kati ya China na Afrika Kusini, na pia ni kumbukumbu ya miaka 35 ya kuanzishwa kwa uhusiano kati ya CPC na ANC. Amesema CPC iko tayari kushirikiana na ANC kuimarisha ziara za viongozi wa ngazi za juu na kuongeza ushirikiano wa kina wa pande nyingi ili kuchangia zaidi kwenye hatma ya pamoja ya jamii ya China na Afrika.

    Kwa upande wake, Magashule amesema ANC inatoa umuhimu mkubwa katika uhusiano wake na CPC, na kwamba anatumai kuwa pande zote mbili zitakuwa na mawasiliano zaidi kwa faida ya watu wa nchi zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako