• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya Umoja wa Mataifa yasema, hali ya umaskini na ukosefu wa usawa nchini Marekani ni mbaya

    (GMT+08:00) 2018-06-05 19:16:33

    Mwandishi maalumu wa kamati ya haki ya binadamu ya Umoja wa Mataifa anayeshughuliki umaskini uliokithiri na suala la haki za binadamu Bw. Philip Alston ametoa ripoti mpya ikisema, hali ya umaskini na ukosefu wa usawa nchini Marekani ni mbaya na inaendelea kuwa mbaya zaidi.

    Ripoti hiyo imesema, kwa mujibu wa takwimu mpya, robo ya matajiri wakubwa zaidi 2,208 duniani wanaishi nchini Marekani. Mali za asilimia 1 ya wamarekani matajiri zaidi inaendeleza kuongezeka, huku mali na mapato ya watu wa kawaida wanaochukua asilimia 90 ya watu wote wa Marekani ikionesha mwelekeo wa kupungua katika miaka 25 iliyopita.

    Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa mwaka juzi asilimia 18 ya watoto nchini Marekani wanaishi katika umaskini. Wakati huohuo, kiwango cha vifo vya watoto wachanga ni zaidi ya maradufu ya kiwango hicho katika nchi nyingine zilizoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako