• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania : Serikali kuu kupiga kilimo jeki.

    (GMT+08:00) 2018-06-05 20:44:13

    Serikali kuu ya Tanzania imetenga shilingi trilioni 13.8 kwa ajili ya kuinua kilimo kote nchini. Mpango huo wa miaka 10 unaoitwa programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo Awamu ya pili, unalenga kuongeza uzalishaji wa tija.

    Akizindua mradi huo jijini Dar Es salaam, Rais John Magufuli alisem akuwa ni matamanio yake kuona kuwa kilimo kinaongezeka haswa katika maeneo madogo. Mradi huu ambao tayari umetengewa shilingi trilioni 2.6 katika mwaka huu wa fedha utasaidia katika usambazaji wa pembejeo kwa wakulima.

    Mradi huu unalenga kuwatoa wakulima wadogo katika kilimo cha kujikimu na kuwaingiza katika kilimo cha biashara kwa kuendeleza na kuchochea ukuaji wa sekta. Fedha hizo zitaelekezwa kwenye miradi 56, iliyogawanywa kwenye makundi manne. Maeneo hayo ni usimamizi endelevu wa matumizi ya maji na ardhi, ambayo itagharimu shilingi trilioni 2; kuongeza tija na fidia katika kilimo. Mifugo na uvuvi itachukuwa shilingi trilioni 8. Biashara na kuongeza thamani ya mazao ni trilioni 3.5 na kuiwezesha sekata katika uratibu, ufatiliaji na tathmini ni shilingi bilioni 137.4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako