• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dar: Gawio la hisa NMB lapungua kwa shilingi 40.

    (GMT+08:00) 2018-06-05 20:44:49

    Baada ya Benki ya NMB kushuhudia kupunguwa kwa faida mwaka wa 2017, bei ya gawio kwa kila hisa imepungua kutoka shilingi 104 iliyotolewa mwaka wa 2016, hadi shilingi 64. Athari hii kwa wanahisa inatokana na misuko misuko mingi iliyoshuhudiwa kwenye Benki ya NMB mwaka jana.

    Kulingana na Ineke Bussemaker, ambaye ni mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki hiyo, mojawapo ya hali ngumu waliyopitia mwaka jana ni kuongezeka kwa mikopo chechefu. Kulingana na Ineke, mikopo chechefu ilichangia asilimia 12 kwenyue sekta huku benki ya NMB ikifikisha asilimia 6.4.

    Kwenye nkutano uliowaleta pamoja wanahisa wa benki hiyo, shilingi bilioni 32 zilipitishwa kwa ajili ya gawio zilizopungua kutoka shilingi bilioni 52 mwaka wa 2016. Hali hii vile vile imeathiri fedha za benki hii ambapo faida imepungua kwa kiwango kikubwa sana kutoka shilingi bilioni 154 mwaka wa 2016 hadi shilingi bilioni 93 mwaka wa 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako