• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Iraq yaidhinisha mapendekezo ya kuchunguza udanganyifu kwenye uchaguzi wa wabunge

    (GMT+08:00) 2018-06-06 09:32:16

    Serikali ya Iraq imeidhinisha mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya ngazi ya juu kuchunguza tuhuma za udanganyifu na ukiukaji kanuni kwenye uchaguzi wa wabunge uliofanyika Mei 12. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya waziri mkuu wa Iraq Bw. Haider al-Abadi inasema Baraza la mawaziri limepitisha mapendekezo yakiwemo kuhesabu upya isiyopungua asilimia 5 za kura kwenye vituo vyote vya kupigia kura, na kufuta matokeo ya kura zilizopigwa nje ya nchi. Taarifa inasema baraza hilo limeamuru mamlaka za sheria kuwafungulia mashtaka watuhumiwa, na kuwazuia maofisa waandamizi wa Tume ya uchaguzi kutoka nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako