• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia kuwahamishia wakimbizi wa DRC kwenye makazi ya kudumu kabla ya Julai

    (GMT+08:00) 2018-06-06 09:52:01

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limesema serikali ya Zambia inatarajia kuwahamisha wakimbizi wote kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo waliopo kwenye kituo cha muda kwenye eneo la Nchelenge mkoani Luapula, kwenda kwenye kituo cha kudumu kabla ya mwisho wa mwezi Julai.

    Zambia ilifungua kituo cha muda cha Kenani mwezi Agosti mwaka jana, ambacho kwa sasa kimewaandikisha wakimbizi zaidi ya 15,000 kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

    Lakini mjumbe maalum wa UNHCR amesema hadi kufikia tarehe 31 Mei wakimbizi 6,621 walikuwa wamepelekwa kwenye makazi ya kudumu ya wakimbizi ya Mantapala.

    Kwa sasa Zambia inahifadhi watu elfu 70 wakiwa ni wakimbizi na watu waliomba hifadhi kutoka nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako