• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yapata dola za Marekani milioni 373 kutokana na mauzo ya madini mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-06-06 10:08:10

    Serikali ya Rwanda imesema mwaka jana ilipata dola za Marekani milioni 373 kutokana na mauzo ya madini, kiasi ambacho kimepita lengo lake la dola za Marekani milioni 240.

    Ofisa Mkuu wa Bodi ya Migodi, mafuta na gesi ya Rwanda Bw Francis Gatare, amesema mafanikio hayo yanatokana na ongezeko la bei ya bidhaa duniani, hasa bidhaa za dhahabu na vito. Pia amesema, mwaka kesho sekta ya madini ya Rwanda inalenga kupata dola za Marekani milioni 600 katika mauzo ya madini.

    Habari zinasema Rwanda inapanga kuanzisha viwanda viwili vya kutengeneza madini ya bati na coltan na kutumia teknolojia mpya ya kusafisha madini ili kuongeza thamani ya bidhaa za madini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako