• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ufaransa asisitiza ahadi kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran

    (GMT+08:00) 2018-06-06 10:09:14

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amemwambia waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu ambaye yuko ziarani barani Ulaya, kuwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 yanapawa kudumishwa, la sivyo usalama wa Israel na mashariki ya kati utakuwa hatarini.

    Hata hivyo rais Macron amesema Ufaransa bado haijaridhika vya kutosha na makubaliano hayo, ambayo ameyaona kuwa ni hatua ya kwanza na yanahitaji kuboreshwa kulingana na shughuli nyingine za baada ya mwaka 2025.

    Rais Macron ametoa wito kwa wenzi na washirika wake kuzingatia juhudi zao za kuhimiza utulivu wa kikanda kwa kudumisha makubaliano hayo, ambayo yameruhusu usimamizi wa shughuli za Iran.

    Wakati huohuo, msemaji wa Tume ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Bunge la Iran Hossein Naqavi Hosseini, amesema ana mashaka kuwa mazungumzo kati ya Iran na nchi za Ulaya kuhusu makubaliano hayo yanaweza kupata matokeo chanya. Amesema Iran haipaswi kupoteza muda kusubiri hatua zinazohitaji kuchukuliwa na serikali za nchi hizo.

    Iran sasa inajadiliana na nchi za Ulaya kwa lengo la kulinda makubaliano ya nyuklia baada ya Marekani kujitoa mwezi Mei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako