• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala cha Ethiopia chaahidi kutekeleza makubaliano ya amani na Eritrea

    (GMT+08:00) 2018-06-06 10:09:39

    Kamati tendaji ya chama tawala cha Ethiopia People's Revolutionary Democratic Front EPRDF imeahidi kutekeleza bila sharti makubaliano ya amani na nchi yake adui Eritrea, yaliyosainiwa mwaka 2001 mjini Algiers na kuipa Eritrea mji muhimu wa Badme.

    Mgogoro wa mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea ulizusha vita vya miaka miwili kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2000, na kusababisha vifo vya watu elfu 70 katika nchi hizo mbili.

    Tangu wakati ule, nchi hizo mbili zimekuwa zikivutana kuhusu mpaka. Ethiopia imekuwa ikisisitiza hitaji la kujadiliana na Eritrea kwanza kabla ya kutekeleza makubaliano ya amani ya Algiers.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako