• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Afrika Mashariki na Kati: CECAFA Kagame Cup kufanyika Tanzania, Juni 28-Julai 13

    (GMT+08:00) 2018-06-06 10:11:20

    Baraza la vyama vya mpira wa miguu vya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, jana limepanga na kutangaza makundi rasmi, pamoja na ratiba ya mechi za kombe la kutafuta klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup).

    Mashindano hayo mwaka huu yanafanyika Dar es Salaam nchini Tanzania kuanzia juni 28 hadi julai 13.

    Jumla ya timu 12 zinazoshiriki michuano hiyo, zimegawanywa katika makundi matatu kama ifuatavyo;

    Kundi A: Azam FC Tanzania, KCCA ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini

    Kundi B: Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti

    Kundi C: Dakadaha ya Somalia, Saint George ya Ethiopia, Yanga na Simba zote za Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako