• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michuano ya SportPesa Super Cup: Singida United yafuzu nusu fainali

  (GMT+08:00) 2018-06-06 10:13:37

  TIMU ya Singida United imefuzu kwenda Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi iliopata dhidi ya AFC Leopards jana kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

  Singida ilishinda kwa penalti 4-2, kufuatia mechi hiyo kuisha kwa sare ya 0-0 na shujaa wa Singida United alikuwa ni golikipa wake, Manyika Peter aliyeokoa penalti mbili, moja wakati wa dakika 90 za mchezo na nyingine kwenye mikwaju ya kuamua mshindi baada ya sare pamoja na baadhi ya hatari zilizoletwa na AFC Leopards kwenye mechi hiyo.

  Singida United sasa itakutana na Gor Mahia kesho kwenye mechi ya nusu fainali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako