• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Marekani na Korea Kaskazini kukutana katika hoteli ya Capella, Singapore

    (GMT+08:00) 2018-06-06 10:50:45

    Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani na Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, watakutana kwenye hoteli ya Capella iliyoko kwenye kisiwa cha Sentosa nchini Singapore.

    Kabla ya hapo Rais Trump alisema mkutano kati yake na Bw. Kim Jong Un utakuwa ni mwanzo wa kitu kikubwa.

    Wakati mkutano kati ya viongozi hao ukisubiriwa, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo jana alikutana na mwenzake wa Singapore Bibi Vivian Balakrishan na kujadili mambo ya biashara, ushirikiano kati ya Marekani na nchi za ASEAN, na kuhusu mkutano unaotarajiwa kufanyika, kati ya rais Trump na Bw. Kim. Bw. Pompeo ameishukuru Singapore kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano kati ya Rais Trump na Bw. Kim.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako