• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuendelea kuweka shinikizo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-06-06 17:02:29

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, kampeni ya kuongeza shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini itaendelea, ingawa rais Donald Trump wa nchi hiyo amesema kuwa hapendi kutumia neno hilo.

    Msemaji wa wizara hiyo Heather Nauert amesema, kampeni ya vikwazo na shinikizo inaendelea kuwepo, na kusema kampeni hiyo haitaondolewa mpaka pale Korea Kaskazini itakapofuata ahadi yake ya kuharibu silaha zote za nyuklia.

    Msemaji huyo amesisitiza kuwa, Marekani imeendelea kushikilia ahadi yake ya kutokuwa na silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea, na kwamba mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini katika kijiji cha Panmunjom na nchini Singapore yanaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako