• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka pande husika za suala la nyuklia la Iran kuendelea kulinda na kutekeleza makubaliano ya pande zote

    (GMT+08:00) 2018-06-06 18:42:47

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inazitaka pande husika za suala la nyuklia la Iran kuendelea kulinda na kutekeleza makubaliano ya pande zote.

    Hivi karibuni, mwenyekiti wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Ali Akbar Salehi amesema, Shirika hilo litafanya maandalizi ya kuongeza uwezo wa kusafisha uranium, na kwamba tarari nchi hiyo imepeleka barua kuhusu hatua hiyo kwa Shirika la Nishati ya Atomiki la Kimataifa.

    Wakati huohuo, Bi Hua amempongeza waziri wa mambo ya nje ya Ecuador Bibi Maria Espinosa kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa huku akisema, China itashiriki kwenye kazi za baraza hilo na kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi na wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako