• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la wadau wa kupunguza umaskini duniani lafanyika huko Rome

    (GMT+08:00) 2018-06-06 18:44:04

    Kongamano la mwaka 2018 la wadau wa kupunguza umaskini duniani limefanyika huko Rome nchini Italia.

    Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na Kituo cha kimataifa cha kusaidia umaskini cha China na kituo cha habari cha mtandao wa Internet cha China na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka China, Ghana, Kenya, Senegal na wasomi wa vyuo vikuu wa Italia.

    Wajumbe hao walibadilishana uzoefu wa mafanikio ya kusaidia kuondokana na umaskini wa nchi mbalimbali, na kujadili kuhusu kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kupunguza umaskini na kuimarisha ujuzi wa kupunguza umaskini.

    Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya kuondoa umaskini ya baraza la serikali la China Bw. Ou Qingping amesema, baada ya juhudi ya miaka mitano, idadi ya watu wenye hali duni kiuchumi imepungua na kiwango cha umaskini kimepungua kutoka asilimia 10.2 hadi 3.1. Amesema China inapenda kuendelea kufanya mawasiliano ya kina na nchi zinazoendelea, kujifunza kutoka mwingine, ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kazi ya kuondoa umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako