• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Baraza la viwanda na biashara la SCO wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-06-06 19:22:14

    Mkutano wa Baraza la viwanda na biashara wa Shirika la Ushirikiano wa Shanghai SCO umefanyika leo mjin Beijing, na kuwashirikisha watu 300 wakiwa ni pamoja na wajumbe kutoka mashirika ya viwanda na biashara kutoka China, Russia, India, Pakistan, Kazakhstan, Uzbekistan, Tajikistan na Kyrgyzstan.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Naibu mkurugenzi wa Chama cha kuhimiza maendeleo ya biashara cha China Bw. Chen Zhou amesema, anatumaini kuwa sekta ya viwanda na biashara ya nchi wanachama wa SCO zitazidi kuimarisha na kupanua biashara ya jadi, kuhimiza biashara kupata ongezeko kubwa zaidi, kupanua sekta ya biashara, na kuvumbua njia za kufanya biashara ili kuhimiza biashara kupata ongezeko kwa hatua madhubuti kwenye kanda hiyo.

    Naibu mwenyekiti wa Chama cha viwanda na biashara cha Russia Bw. Padalko amesema, Russia inaimarisha ushirikiano wa ujenzi wa miundo mbinu na nchi husika chini ya mfumo wa shirika la SCO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako