• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Viajana kuweweshwa katika sekta ya viwanda

  (GMT+08:00) 2018-06-06 19:44:49

  Wadau wa maendeleo wamewashauri vijana kujiunga na vyuo vya ufundi stadi ili kunufaika na mradi wa mafunzo ya kuboresha ujuzi na kujipatia ajira (ISTEP) uliolenga kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira, umaskini pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Mradi huo wa miaka sita (2014-2020) wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 13 unaodhaminiwa na kutekelezwa na serikali ya Canada kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

  Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano wa Kamati kuu ya ISTEP uliokutanisha wadau kutoka taasisi mbali mbali kujadili mafanikio ya mradi huo.

  Mkurugenzi wa mafunzo na ufundi stadi (TVET) kutoka Wizara ya Elimu, Dk. Noel Mbonde amesema mradi huo umelenga zaidi kuwandaa vijana katika shughuli mbalimbali za kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda.

  Akichangia mafanikio ya mradi, Waziri Mshauri katika ubalozi wa Canada nchini Tanzania, Susan Steffen amesema ISTEP imewajengea wanawake uwezo na ujasiri wa kushiriki shughuli mbali mbali zilizokua zikidhaniwa kuwa ni za wanaume tu.

  Ameongeza kuwa baadhi ya wanawake katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza wamekuwa wakishiriki kazi za kuendesha mashine na mitambo mbali mbali migodini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako