• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EAC:Fursa za kazi za madereva wa kike kupatikana Saudia Arabia

  (GMT+08:00) 2018-06-06 19:45:10

  Huenda wanawake kutoka nchi za Afrika mashariki sasa wakapata fursa za kazi za udereva Saudia Arabia.

  Serikali ya Saudi Arabia imeanza kutoa leseni za kuendeshea magari kwa wanawake wa nchi hiyo, hii ikiwa ni miongo mingi kupita tangu kuanzishwa kwa sheria iliyoharamisha jambo hilo.

  Wiki chache zilizopita, serikali ya nchi hiyo ilifuta sheria ambayo ilikataza wanawake kumiliki leseni na hii inakuja baada ya Mfalme wa nchi hiyo, Salman kutangaza mwaka jana kuwa wanawake wanaruhusiwa kuendesha gari.

  Sheria hiyo mpya ya kutoa leseni hizo kwa wanawake inatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi ingawa tayari baadhi wameanza kupata leseni zao huku wengine wakifanya mchakato wa kuomba.

  Kwa mujibu wa Wizara ya Habari, jumla ya leseni 2,000 zitakuwa zimeshatolewa ifikapo wiki ijayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako