• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwekezaji katika Klabu ya Simba Mohamed Dewji aanzisha tuzo za Simba

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:03:20
    Mwekezaji katika club ya Simba ya Dar es salaam Tanzania, Mohammed Dewji ametangaza rasmi kuwa ameamua kuanzisha tuzo za MO Simba Awards ambazo zitatolewa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa club ya Simba. Kwa mara ya kwanza tuzo hizo zitatolewa siku ya Jumatatu June 11 katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam. Kutakuwa na vipengele 16, ambavyo ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka. Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Shabiki Bora wa Mwaka na Tuzo ya Heshima, Tuzo zingine ni Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka, Tuzo ya Benchi la Ufundi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako